Kikosi cha Pan African kinatarajia kushuka dimbani kesho jumamosi kumenyana na Gwambina kwenye mchezo wa ligi ya Championship.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mej. Generali Isamuhyo.

Pan African, Pan African Kuivaa Gwambina kesho, Meridianbet

Timu hizo zikiwa zimecheza michezo sita ya ligi kwa msimu huu wa 2022/23 tayari Gwambina imekusanya pointi 4 huku Pan wakiwa nazo 3.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema kuwa: “Tunamshukuru Mungu kikosi leo kimefanya mazoezi ya mwisho salama.

“Hatuna majeruhi yeyote kwenye kikosi hivyo ari na morali ni kubwa kuelekea kwenye mchezo huo ukizingatia tumepata benchi jipya la ufundi.

“Mipango ya kocha ni kuanza vizuri kibarua chake kwa ajili ya kuhakikisha Pan African inarudi katika ubora ule ambao watu wengi wanaifahamu timu yetu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa