Pan African Wanazitaka Pointi za JKT

Kikosi cha Pan African kinajiandaa na mchezo wa ligi ya Championship dhidi ya JKT Tanzania kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Iddy Cheche.

Pan walianza mazoezi yao jana jumatatu kwa ajili ya mchezo huo ambao utapigwa Novemba 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Pan African

Pan inashuka kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya Gwambina huku JKT wakitoka sare ya bila kufungana na Green Warriors.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema: “Kikosi chetu kimeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu ujao dhidi ya JKT Tanzania.

“Tunawaheshimu JKT ni timu nzuri ina benchi zuri la ufundi lakini tunachohitaji zaidi ni pointi tatu ambazo zitatuweka sehemu salama kwenye msimamo wa ligi.

“Kocha ameridhishwa na viwango vya wachezaji na amesema kuna baadhi ya vitu vichache vya kuongezea ili timu iwe bora zaidi hivyo wanachama watarajie vitu vizuri zaidi.”

Acha ujumbe