Pan African Wana Jambo Lao Jumamosi

Kikosi cha Pan African kinachoshiriki ligi ya Championship kinatarajia kucheza mechi ya mzunguko wa 10 dhidi ya Copco.

Tangu Kocha Mkuu, Iddy Cheche akichukue kikosi hicho amefanikiwa kupata ushindi katika michezo miwili dhidi ya Gwambina na Fountain Gate huku akipoteza mmoja dhidi ya JKT Tanzania.

Pan African

Akizungumzia maandalizi yao kiufundi, Kocha Msaidizi wa Pan African, Daudi Macha amesema: “Kikosi kinaendelea vizuri na wachezaji wapo fiti kimwili na kiakili kuelekea kwenye mchezo huo.

“Mipango yetu ilikuwa kupata pointi tisa katika michezo mitatu lakini imeshindikana hivyo tumezipata sita na sio mahesabu mabaya sana kwetu.

“Tunaenda Mwanza kuendelea tulipoishia hivyo wapinzani wetu wajiandae kwani tunahitaji pointi tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri.”

Acha ujumbe