KIKOSI cha Pan African kesho jumapili kinatarajia kushuka dimbani kumenyana na Fountain Gate kwenye mchezo wa ligi ya Championship.

Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar huku Pan wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania.

Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema “Maandalizi yamemalizika kuelekea kwenye mchezo wetu wa jumapili dhidi ya Fountain Gate.

“Licha ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania lakini wachezaji wana morali ya kuhakikisha pointi tatu kwenye mchezo huu zinapatikana kwa ajili ya kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

“Wapinzani wetu tunawaheshimu sana kwani wana timu nzuri na benchi zuri la ufundi lakini sisi pia tunahitaji pointi tatu kwani tulizipata mara moja tu tangu kuanza kwa msimu huu.”

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa