Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate kikosi cha Pan African kitarejea mazoezini kesho kujiandaa na mchezo ujao wa Championship.
Pan itashuka tena dimbani Novemba 19 mwaka huu kumenyana na Copco ya Jijini Mwanza kwenye Uwanja wa Nyamagana.
Akizungumza hali ya kikosi chao, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema: “Kikosi chetu kitarejea mazoezini kesho jumanne kujiandaa na mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Copco.
“Tuna furaha sana baada ya kupata ushindi wa jana hivyo kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Copco basi wajiandae na kipigo.
“Mipango yetu inaendelea vizuri na ushindi huu unaongeza morali kwa wachezaji, benchi la ufundi katika kutimiza malengo yetu msimu huu.”