KIKAO maalumu cha wanachama wa Klabu ya Pan African kilichokaa kwa ajili ya kujadili mabadiliko ya katiba kimepitisha katiba yao baada ya kufanya marekebisho. 

Akizungumzia hilo, Katibu wa Kamati ya Marekebisho ya Katiba wa Klabu ya Pan African, Peter Mushi amesema kuwa baada ya mchakato wa awali kupita wanatarajia kukutana tena ili kufanya uchaguzi.

pan, Pan Wapitisha Mabadiliko ya Katiba, Meridianbet

“Marekebisho haya Kwa mara ya kwanza tuliyafanya 2016 bahati mbaya msajili hakuyapitisha akarudisha tena kwetu Kwa ajili ya marekebisho madogo ya kiutawala.

“Makubaliano kwenye mkutano maalumu uliofanyika ukumbi wa Polisi Mess Oysterbay Agosti 13, mwaka huu Kwa kauli moja wanachama wamepitisha Kwa ajili ya kupeleka Kwa Kwa msajili ili aweze kupitisha.

“Baada ya wiki mbili tunaweza kukaa Kwa ajili ya kusoma mapato na matumizi na kuchagua viongozi wapya ambao wataiongoza Pan African Kwa miaka minne ijayo”.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa