Pan yataja sababu za kipigo cha Mbeya Kwanza

Kikosi cha Pan African kinachonolewa na Kocha Mkuu, Iddy Cheche jana jumapili kilipoteza mchezo wa ligi ya Championship dhidi ya Mbeya Kwanza kwa mabao 3-1.

Akizungumzia sababu ya kupoteza mchezo huo, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema kuwa ni kukosekana kwa wachezaji wao nane kwenye kikosi cha kwanza.

Pan yataja sababu za kipigo cha Mbeya Kwanza

“Ni kweli tumepoteza mchezo wetu wa jana dhidi ya Mbeya Kwanza lakini kwa sasa kocha anaenda mazoezini kuyafanyia kazi yale mapungufu aliyoyaona kwenye mchezo huo.

“Tatizo kubwa ni kuwakosa wachezaji wetu nane ambao walikuwa kwenye kikosi cha kwanza ambapo sita walisimamishwa, na wawili walikuwa wagonjwa hivyo hawakuwepo kwenye mchezo wa jana.”

Acha ujumbe