KLABU ya Azam FC inafanya mabadiliko makubwa ya kikosi chao na kinachoendelea kwa sasa kwao ni kuwaacha wachezaji ambao wameonekana kutokuwa na msaada kwao. Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali.
Keneth Muguna ni miongoni mwa nyota ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu wa 2023/24.
Raia huyo wa Kenya hajawa na msimu bora ndani ya 2022/23 kutokana na kushindwa kuonyesha makeke yake. Ukiwa na meridianbet unapata odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.
Ni shuhuda wa timu hiyo ikipoteza mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation kwa ubao wa Uwanja wa Mkwakwani kusoma Azam FC 0-1 Yanga.
Pia Rodgers Kola naye ambaye ni mshambuliaji raia wa Zambia naye pia hatakuwa kwenye kikosi hicho.

Mwingine ni Bruce Kangwa ambaye alijiunga na timu hiyo 2016. Wengine ni Cleofas Mkandala, Ismail Azizi Kada, kocha Kali Ongala na kocha wa makipa Dani Caneda.
Nabi hana deni mwacheni aende salama
NCHI na hususan tasnia ya michezo nchini Tanzania imetikisika kwa taarifa kubwa ambayo ilianza kama tetesi ya kuondoka kwa kocha wa Yanga, Nasredin Nabi.
Jana usiku, klabu ya Yanga ilitoa taarifa ya kuwa wamefikia makubaliano na kocha Nabi ya kumruhusu aondoke baada ya kuomba kuondoka na kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.
Hivyo ni kuwa rasmi mwamba aliyetikisa Tanzania na Afrika kwa misimu miwili anaondoka kwenye jezi za njano na kijani. Hazikuwa taarifa nzuri kwa mashabiki wa Yanga hata kidogo.
Ingawa utofauti wa mapokeo ulikuwa ni kwa upande wa mashabiki wa Simba ambao wao walizipokea kwa furaha sana taarifa za kuondoka kwa Nabi. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Hakika hata sisi tunakubali kuwa ni pigo kwa Yanga na mpira wa Tanzania, kwa kuwa tunaamini kuwa kwa kile ambacho amekifanya kimeacha alama kubwa kwenye mpira wa Afrika.
Mashabiki na wao wanapaswa wakubaliane na kila kitu ambacho kimetokea kwao. Maisha ya mpira ndivyo yalivyo kuna watu wanakuja na kuondoka, hakuna mchezaji au kocha atakayedumu milele.
Alex Ferguson na Arsene Wenger walikaa Man U na Arsenal na wakaondoka. Wakubaliane na hali halisi. Nabi ameondoka na Yanga bado ipo na itazidi kuendelea.
Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.


