Phiri nje wiki moja

Nyota wa kikosi cha Simba, Moses Phiri ambaye alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar atakuwa nje ya kikosi kwa wiki moja.

Nyota huyu ndiye kinara wa mabao katika kikosi cha Simba ambapo tayari amefunga mabao 11 kwenye ligi.

Phiri nje wiki moja

Akizungumza baada ya kutua Jijini Dar, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa “Wachezaji wetu watakuwa kwenye mapumziko leo na kesho watarejea kambini kwa ajili ya kuendelea na mazoezi.

Phiri nje wiki moja

“Ripoti ya dokta imeeleza kuwa nyota huyo atakuwa nje ya uwanja kwa wiki moja ambapo atakosa michezo miwili, ule wa jana dhidi ya KMC na Tanzania Prisons.

“Phiri ataanza mazoezi hivi karibuni hivyo tutakuwa naye kwenye safari ya kuelekea Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.”

Acha ujumbe