ALIYEPELEKA kilio kwenye klabu ya Nyasa Big Bullets kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika raia wa Zambia Moses Phiri, alisema kuwa kiungo wa timu hiyo Clatous Chama ndiye msuka mipango ya magoli yake ya yote.

 

Phiri: Yule Chama ni Master Kabisa

Phiri alifunguka kuwa Chama ni master kweli linapofika suala la kupika mabao, na kama akiwa na mpira mguuni na wewe kama mshambuliaji unachotakiwa kufanya, ni kuingia kwenye boksi na kusubiri pasi ya mwisho.

 

Phiri: Yule Chama ni Master Kabisa

Phiri ambaye anacheza msimu wake wa kwanza ndani ya Simba SC akitokea Zanaco FC ya Zambia, amefunga mabao matatu kati ya manne ambayo yamewavusha Simba SC Kwenda hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 4-0, wakishinda 2-0 kila mchezo wa nyumbani na ugenini.

“Siri ya mabao yangu ni kazi ya pamoja ambayo inafanywa na wachezaji wenzangu wa Simba na maelekezo mazuri ya kocha wetu. Lakini Chama ndiye master wa kila kitu kwa sababu ni mtu ambaye akiwa na mpira mguuni.
 
 “Wewe kama mshambuliaji unatakiwa kwenda kwenye boksi na kusubiri pasi ya mwisho na huyo ndiyo Chama,” alisema.

Simba watakutana na Primeiro do Agosto ya Angola, wakianzia ugenini Oktoba 8 na kisha kucheza nyumbani Oktoba 15 mwaka huu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa