Polisi: Tumekuja kivingine mzunguko wa pili

Kuelekea kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu uongozi wa Polisi Tanzania umefunguka kuwa kwa sasa wamekuja kivingine.

Timu hii inatarajia kucheza kesho jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar dhidi ya Yanga.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chao, Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania, John Tamba amesema “Kiufundi tumeandaa timu vizuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho ambapo tayari wachezaji wapo vizuri kimwili na kiakili.

Polisi: Tumekuja kivingine mzunguko wa pili

 

“Tumefanyia marekebisho yale mapungufu yote yaliyojitokeza kwenye raundi ya kwanza hivyo tuna imani kesho tutapata ushindi kwenye mchezo huo.

“Kikubwa mashabiki wetu waendelee kutupa sapoti kwani katika mzunguko huu wa pili tumekuja kivingine kwa ajili ya kuhakikisha tunakuwa kwenye nafasi nzuri.”

Acha ujumbe