Klabu ya Polisi Tanzania imemtangaza kocha mkuu mpya wa ambaye ataingoza klabu hiyo kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza hivi karibu kutoka nchini Burundi Joslin Sharif kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Joslin anajiunga na Polisi akiwa mbadala wa aliyekuwa Kocha Mkuu, Malale Hamsin ambaye mkataba wake ulisitishwa hivi karibuni kwa makubaliano ya pande zote.

Polisi Tanzania, Polisi Tanzania Yashusha Kocha Kutoka Burundi, Meridianbet

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Polisi Tanzania imeeleza kuwa Kocha huyo ana leseni ya daraja A inayotambulika na Shirikisho la Soka Afrika, (CAF) na Diploma ya ukufunzi.

“Polisi Tanzania imeingia makubaliano nae baada ya kupitia CV za makocha mbalimbali na kuridhishwa na CV ya Joslin ambaye kwa nyakati tofauti amecheza mpira kwenye vilabu vya OC Muungano ya DRC, MP FC, Kibuye FC, KIST FC za Rwanda, Atheletico na Vitalo za Burundi.

“Aidha amecheza kwenye timu ya taifa ya Burundi na kufundisha timu ya taifa ya nchi hiyo ikiwemo ya U23. Kwa upande wa vilabu amefundisha Bumamuru FC, Messager Ngozi na Aigle Noir za nchini Burundi.”


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa