Uongozi wa Klabu ya Polisi Tanzania umeweka wazi kuwa wataweka Kambi maalumu kwa ajili ya maandalizi ya michezo inatayotarajia kuanza hivi karibuni kwenye msimu wa 2022/23 katika jiji la Dar es Salaam.

Ofisa habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa klabu hiyo, wanatarajia kusafiri kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka kambi ya siku kadhaa ili kuwasaidia kuwaweka sawa kimbinu na kiakili wachezaji wao na kuwa karibu na mashabiki wao wa mkoa huo kwa ajili ya msimu ujao.

Polisi Tanzania

“Tunaweka kambi Dar kwa sababu kuna mashabiki wetu wengi na kuna hali ya hewa nzuri hasa ukizingatia kwamba sisi tuna mashabiki kila mahali kwa hapa Tanzania, jambo ambalo limefanya tuweze kufikiria kuweka kambi Dar.

“Hata hivyo kwa upande wa hali ya hewa ni shwari na kumetulia tutafanya maandalizi ya kutosha ili tulete ushindani mkubwa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa