ALLY Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapinzani wao Polisi Tanzania wanawafuata machinjioni Uwanja wa Mkapa jijini Dar hivyo wajiandae ‘kufa’.

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ikiwa imekusanya pointi 38 baada ya kucheza mechi 15 mchezo wake uliopita Uwanja wa Mkapa ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho na iliibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Kurugenzi.

Polisi Tanzania wameyakanyaga kwa Yanga

Timu hiyo inanolewa na Mwinyi Zahera ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Yanga ambacho kwa sasa kipo chini ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.

Kamwe amesema: “Jumamosi tunacheza na Polisi Tanzania, wanakuja machinjioni hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani na tunaamini kila kitu kitakuwa sawa.”

Polisi Tanzania wameyakanyaga kwa Yanga

Mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ubao ulisoma Polisi Tanzania 1-2 Yanga.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamefanya mazoezi ya mwisho ni pamoja na Eric Johora, Kibwana Shomari, Dickson Job.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa