Klabu ya Polisi Tanzania imejikuta ikikalia kuti kavu baada ya kupoteza alama tatu wakiwa nyumbani katika dimba lao wanalotumia kwasasa la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Klabu ya Polisi Tanzania imepoteza mchezo kwa kufunga bao moja kwa bila dhidi ya klabu ya Mbeya City kutoka jijini Mbeya, Bao pekee lililopeleka kilio kwa maafande lilifungwa na mshambuliaji wa Mbeya City Tariq Seif mapema katika dakika ya nane ya mchezo huo.polisi tanzaniaKlabu ya Mbeya City wanapata matokeo ugenini hii inadhihirsha namna ambavyo klabu hiyo kutoka manispaa ya Jiji la Mbeya imekua kwenye wakati mzuri tofauti na mwanzo wa msimu, Klabu hiyo ya Mbeya pia inafanikiwa kusogea katik msimamo wa ligi kuu ya NBC.

Polisi Tanzania baada ya kupoteza mchezo wa leo wameendelea kukaa nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC, Kwani klabu hiyo kabla ya mchezo wa leo ilikua nafasi ya 15 katika msimamo wakiwa na alama 19 na baada ya mchezo wa leo wameendelea kukaa palepale na alama zao zilezile.polisi tanzaniaWakati Mbeya City wakiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kufikisha alama 27, Polisi Tanzania ambao wamepoteza mchezo wa leo wameendelea kukaa nafasi ya 15 nafasi moja kutoka anaeshika mkia ambaye ni klabu ya Ruvu Shooting jambo ambalo sio nzuri kwa klabu hiyo kwani ikiendelea hivi ni wazi watashuka daraja msimu huu.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa