Baada ya kuanza vibaya msimu huu wa 2022/23, Uongozi wa Polisi Tanzania umefunguka kuwa usajili waliofanya ni kwa ajili ya kubaki ligi kuu kwa msimu ujao.
Polisi Tanzania chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera wapo nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 19 na kukusanya pointi 11.
Katibu Mkuu wa Polisi Tanzania, Robert Munisi amefunguka kuwa “Sisi tupo ICU tunatakiwa kupata nafuu na kwenda wodini na baadae tutoke hospitali.
“Kuachana na Vitalis Mayanga ni jambo sahihi kwa upande wetu kwani katika michezo sita aliyocheza amefungua mabao mawili pia Polisi hatujawahi kumng’ang’ania mchezaji.
“Tayari tumefanya usajili wa wachezaji kama Kelvin Sabato, Ramadhan Chombo Redondo, Mohamed Issa ‘Banka’ na straika mmoja kutoka Congo na usajili huo ni kutokana na mapendekezo ya kocha.
“Tunataka kuleta vitu vya uhakika kwani mwanzoni tuliteleza hivyo bado tuna dhamira ya kucheza ligi kuu kwa msimu ujao.”