RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezitaka klabu za Simba na Yanga na zote ambazo zinashiriki mashindano ya kimataifa, kuhakikisha zinafanya vema na kufika mbali zaidi katika mashindano hayo.

 

Rais Samia Ataka Simba, Yanga Zitishe Kimataifa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mohamed Mchengerwa, ambaye aliagizwa na rais kwenda kushuhudia mechi mbili za Simba na Yanga zilizochezwa wikiendi iliyopita na kisha kuzungumza na wachezaji.

 

Rais Samia Ataka Simba, Yanga Zitishe Kimataifa.

Mchengerwa alisema aliagizwa na Rais Samia kumuwakilisha kuitazama mechi za Simba SC na Yanga SC, na kupata nafasi ya kuwapa ujumbe wa rais wachezaji ambao unawataka kupambana zaidi na kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ili wafike mbali.

“Nilikuja kutazama mechi za Simba na Yanga za kimataifa kwa agizo la rais na nilipata nafasi pia ya kuzungumza na wachezaji wote baada ya mechi, kubwa rais amewapongeza kwa kufanya vizuri kwenye mechi zao zote.
 
“Rais Samia, amewataka wachezaji wote kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi na kufika mbali katika mashindano haya ya kimataifa na kuendelea kuitangaza nchi yetu,” alisema.


Simba SC na Yanga SC zimetinga kwa kishindo kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kishindo, Yanga wao wataanzia nyumbani kucheza dhidi ya Al Hilal ya Sudan Oktoba 8. Huku Simba wao wataanzia ugenini kule Angola kucheza na Premiero do Agosto.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa