RAIS SAMIA AWAPELEKA MASHABIKI YANGA SOUTH AFRICA

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan itagharamia safari nzima ya mashabiki 48 wa Yanga kwenda Pretoria, Afrika Kusini kushuhudia mechi ya marudiano baina ya Mamelodi Sundowns na Yanga itakayochezwa, Ijumaa, Aprili 5 katika Uwanja wa Loftus Versfeld.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema kuwa serikali imeamua kufanya hivyo ili kama sehemu ya mchango wa kuhakikisha timu hiyo inafanya vyema katika mechi hiyo na kuonyesha sapoti yake katika maendeleo ya michezo nchini.RAISMashabiki hao 48 wameanza safari leo wakipita nchi ya Zambia, Zimbabwe na kuingia Afrika Kusini na wanatarajia kuwasili kwenye mji wa Pretoria kesho kutwa tarehe 4.

“Safari hii itakayowawezesha wapenzi hawa kindakindaki wa Yanga kuishangilia timu yao mubashara wakiwa uwanjani imegharimiwa kwa asilimia mia na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo na kutoa ushirikiano kwa uwekezaji binafsi kwenye sekta ya michezo,” alisema Mwana FA.

Fedha ambazo serikali itagharamia ni za safari na pia zile za kujikimu.
Hii ni mara ya pili kwa serikali kufanya hivyo kwa klabu ya Yanga ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka jana ilipogharamia safari ya mashabiki wa timu hiyo kwenda kushuhudia mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya timu hiyo na Marumo Gallants ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.RAIS“Asubuhi hii nimeshiriki kuwaaga wapenzi 48 wa klabu ya Yanga ambao wanaanza safari yao leo kwa basi kuelekea Pretoria, Afrika ya Kusini kushuhudia mchezo wa marudiano wa timu yetu hii dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaochezwa Ijumaa ya tarehe 05/04.

Acha ujumbe