Ratiba ya Ligi ya NBC Premier League Yatoka Simba na Yanga ni Oktoba 19

Hatimaye baada ya kusubiri kwa hamu ratiba ya ligi kuu ya NBC, leo hii imetoka ambapo mechi zitaanza kuchezwa kuanzia 16 Agosti.

Ratiba ya Ligi ya NBC Premier League Yatoka Simba na Yanga ni Oktoba 19

Mechi ya kwanza ya ufunguzi wa ligi kuu itakuwa ni mechi ya Pamba dhidi ya Tanzania Prisons katika dimba la CCM Kirumba. Mwenyeji amepanda ligi kuu msimu huu baada ya kucheza ligi daraja la kwanza kwa muda mrefu.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Bingwa mtetezi wa NBC Premier league mara tatu mfululizo, Yanga yeye ataanzia ugenini dhidi ya Wanankurukumbi Kagera Sugar mchezo ambao utapigwa katika dimba la Kaitaba majira ya saa 1:00 usiku.

Ratiba ya Ligi ya NBC Premier League Yatoka Simba na Yanga ni Oktoba 19

Wakati kwa upande wa Simba yeye ataanzia nyumbani dhidi ya Tabora United ambao walinusurika kushuka daraja msimu uliopita. Mchezo huo utapigwa majira ya saa 10:15 jioni katika dimba la KMC Complex pale Mwenge.

Ikumbukwe kuwa Mnyama atautumia uwanja wa KMC kama uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubaliwa na Bodi ya ligi.

Huku Azam FC wao ambao walimaliza nafasi ya pili, wataanza kugombani ubingwa msimu huu dhidi ya JKT Tanzania ugenini katika dimba la Meja Jenerali Isamhiyo majira ya 10:00 jioni.

Ratiba ya Ligi ya NBC Premier League Yatoka Simba na Yanga ni Oktoba 19

Nao KMC ambao wamedhaminiwa na kampuni kubwa ya ubashiri Tanzania Meridianbet wao wataanza mechi ya kwanza tarehe 19 dhidi ya Coastal Union ambao wao walimaliza nafasi ya 4 kwenye ligi.

Vilevile, ile dabi ya Kariakoo yaani Simba na Yanga wamepangwa kukutana Oktoba 19, huku mnyama ndiye ambaye atakuwa mwenyeji wa michuano hiyo.

Je kwa usajili ambao timu zimefanya msimu huu nani atakuwa bingwa?. Au Yanga ataendeleza ubabe wake mbele ya timu zingine kwa mara ya 4?

Acha ujumbe