Red Arrows Waalikwa Kucheza na Yanga

KLABU ya Yanga hadi sasa haijaanika jina la timu itakayoshiriki tamasha la Siku ya Mwananchi itakayofanyika Kwa Mkapa, siku moja baada ya Simba Day lakini kwa taarifa tulizozipata Meridianbet Sports ni kwamba watacheza na Red Arrows Mabingwa wa Zambia na Kagame Cup 2024. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Hata hivyo chanzo kutoka klabu ya Yanga kilipotafutwa, hakikutaja jina la timu hiyo na kudai kuwa wamepanga kufanya sapraizi.

“Hadi sasa jina la timu ni siri na itatolewa kama sapraizi, kama ilivyokuwa kwa jezi. Bahati nzuri tiketi za tamasha zimeanza kununuliwa na nyingine kuisha kabisa, msiwe na hofu. Bado kuna muda wa maandalizi ya tamasha na jina litaanikwa tu,” Kilisema chanzo kutoka ndani  ya Yanga.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Msimu uliopita katika tamasha hilo, Wananchi iliialika Kaizer Chief na kuifunga bao 1-0, lililowekwa kimiani na Mzambia, Kennedy Musonda ambaye bado yupo kikosini na jana alianzia benchini wakati timu hiyo ikiumana na Amakhosi kuwania Kombe la Toyota.

Yanga ilianzisha tamasha hilo mwaka 2019 ikifuata nyayo za Simba walioasisi Simba Day mwaka 2009 chini ya uongozi wa Hassan Dalali na Mwina Kaduguda na safari hii itakuwa ni msimu wa sita kwa Yanga.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Acha ujumbe