HIVI HAMUOGOPI? Kule Clatous Chama, Huku Aziz Ki, Hapa Pacome, pembeni Maxi Nzengeli hatimaye yametimia waliyokuwa wanayasubiri Wananchi, Chama sasa ni rasmi mali ya Yanga. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Baada ya kutambulishwa Yanga, Chama anaingia kwenye orodha ya wachezaji waliowahi kucheza timu zote mbili, Simba na Yanga.
Amewahi kufanya hivyo Haruna Niyonzima, Amis Tambwe, Emmanuel Okwi, Kelvin Yondani, Juma Kaseja, Ivo Mapunda, Jonas Mkude,Gadiel Michael, Bernard Morrison, Ibrahim Ajibu, Augustine Okrah na wengine wengi.
Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.
SAKATA LAKE HADI KUSHINDWANA NA SIMBA
Baada ya kurejea nchini akitokea kwao nchini Zambia Clatous Chama aliitwa na Bosi Dubai ambako alikwenda kwa mazungumzo baada ya kufika Dubai Chama aliongeza Dau kutoka pesa aliyokuwa anaitaka hapo mwanzo na kutaka apewe dolla 350 sana na zaidi ya milioni 800 ili asaini Simba.
Clatous Chama pia alihitaji mshahara wa zaidi ya milioni 40 kwa mwezi ili asalie ndani ya Simba Mo Dewji na kamati yake wakaona anafanya hivyo kwa sababu ya ofa ambayo ipo mezani kwake ya kutoka Yanga.
Leo Clatous Chama ametambulisha kujiunga na Yanga kwa Dolla 350 sawa na zaidi ya milioni 820 za Kitanzania huku atakuwa akilipwa mshahara wa kiasi cha milioni 35 kwa mwezi mmoja na kuwa mchezaji wa pili anayelipwa pesa nyingi katika timu hiyo baada ya Azizi Ki.
TAKWIMU ZA CHAMA LIGI KUU AKIWA SIMBA
MECHI: 139
MAGOLI: 27
ASSISTS: 54
TAKWIMU ZA CHAMA CAF AKIWA SIMBA
MECHI: 44
MAGOLI:15
ASSISTS:6
Chama anaondoka SIMBA baada ya kudumu kwa miaka mitano na nusu alijiunga SIMBA 2018 akitokea Power Dynamos ya Zambia.
Ilikuwa ni ndoto ya mashabiki na wapenzi wa Yanga kuona mchezaji huyo anavaa jezi yao na kukipiga mitaa ya Jangwani, na hatimaye ndoto imekuwa kweli msimu ujao 2024/25 Chama atasambaza pasi za upendo mitaa ya Jangwani.
Pembeni yake kutakuwa na Pacome, kule Maxi Nzengeli, huku Aziz Ki, huenda Yanga sasa ikazidi kufanya vizuri zaidi kwenye soka la ndani na la Kimataifa.
Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.