KOCHA wa Simba Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema, anachohitaji ni kuwafunga Al Ahly kesho na kuweka heshima na rekodi Afrika kwa kumsimamisha kigogo wa soka la Afrika kwenye mechi ya kwanza ya African Football League.

Robertinho na Simba yake, kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar wanakutana na mpinzani mgumu Al Ahly, wanamheshimu lakini kwa sasa kila mpinzani anapaswa kuiheshimu Simba pia.

“Tuna timu nzuri, tunaheshimu kila mpinzani aliyepo mbele yetu, kesho ni fursa nzuri kwa wachezaji wangu kucheza mechi kubwa. Tunaiheshimu Al Ahly kwa sababu ina wachezaji wengi wenye uzoefu mkubwa lakini pia kila timu inapaswa kuiheshimu Simba.”

“Kama nilivyosema awali Al Ahly ni timu kubwa, ina mafanikio zaidi Afrika lakini kesho tunahitaji kuonesha uwezo wetu. Kwangu mchezo wa mpira wa miguu sio kama kupigana bali ni sanaa, kesho itakuwa ni mechi nzuri,” alisema.


Robertinho, aliwataka mashabiki wa Simba kuwa tayari kwa mchezo huo na wanapaswa kwenda kwa wingi kwenye Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya mchezo huo mkubwa Afrika na dunia ya soka.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa