HUKU zikiwa zimesalia siku 8 kabla ya kuwavaa na Al Ahly katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya mashindano ya African Football League, Kocha Mkuu wa Simba Mbrazili, Robert Olivieira ‘Robertinho’ amechimba mkwara mzito kuwa watakuwa na programu nzito ya siku nne kuhakikisha wanapata matokeo katika mchezo huo.

Mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Fountain Gate, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Jumapili iliyopita kikosi cha Simba kimepewa mapumziko mafupi ya kupisha kalenda ya michezo ya kimataifa.robertinhoRobertinho ambaye amewapa programu maalum wachezaji wa timu hiyo kuifanya wakiwa nyumbani amewatangazia wachezaji kuwa mara moja watahitajika kambini mara baada ya ratiba hiyo ya kimataifa kukamilika.

Robertinho alisema: “Kwa sasa kikosi kinatarajiwa kuwa na mapumziko mafupi ya kupisha Kalenda ya FIFA ambayo inaanza Oktoba 9-17, ambapo tumewapa program maalum ya kufanya wakiwa kwenye mapumziko hayo.robertinho “Baada ya ratiba ya FIFA kumalizika kikosi kitarejea haraka kambini kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa African Football League dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Oktoba 20.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa