KOCHA wa Simba Robertinho amesema kuwa kuelekea katika mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Ihefu wanatarajiwa kuucheza kwa umakini mkubwa kutokana na kueekea katika mchezo wa derby dhidi ya Yanga.
Simba leo Jumamosi wanatarajiwa kumenyana na Ihefu katika mchezo wa ligi kuu unaotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Mkapa.
Robetinho alisema kuwa “Tunakwenda kuucheza mchezo huu tukiwa na tahadhari kubwa kuelekea katika mchezo wetu wa ligi mwingine dhidi ya Yanga.
“Ni mchezo mkubwa sio Tanzania tu bali ni mchezo mkubwa Afrika nzima hivyo lazima tulitambue hilo kwa kufanya maandalizi mzuri kwa kuwa malengo yetu ni kuona kuwa tunapta matokeo katika michezo yote.“Hatutakiwi kuwa na wasiwasi bali tunatakiwa kufanya matayarisho mazuri,wachezaji wangu nawaamini kwa kuwa nafahamu kuwa wana uwezo mkubwa na watatufanya tupate matokeo katika michezo yetu hii miwili ya mbele yetu,”alisema kocha huyo