‘Robertinho’ Mbrazil, Roberto Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba, amesema wachezaji wake wapya, Ismael Sawadogo na Jean Baleke, wamekosa fitinesi pekee ambayo amepanga kuwaongezea, lakini katika suala la kiwango, wapo vizuri.
Hiyo ni baada ya juzi kocha huyo kuwatumia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa Uwanja wa Jamuhuri, Dodoma.
Katika mchezo huo, Baleke alifunga bao lililoipa pointi tatu Simba wakishinda 0-1.
Robertinho, alisema wachezaji wake hao wapya wamecheza vizuri tofauti na matarajio yake kwa kila mmoja kucheza kwa kufuata maelekezo aliyowapa.
Robertinho alisema kikubwa anawapongeza zaidi kwa kuzoea mazingira haraka ambayo yamewafanya kucheza katika kiwango bora wakifanya mazoezi kwa siku mbele pekee.
Aliongeza kuwa kikubwa atakachokifanya hivi sasa ni kuwaongezea fitinesi ambalo ndiyo jukumu lake ili kuhakikisha wanakuwa bora zaidi katika michezo ijayo.
Nimefurahishwa na viwango bora ambavyo wamevionyesha wachezaji wetu ambao tumewasajili katika dirisha dogo.
“Haikuwa rahisi kwao kucheza katika kiwango hicho kikubwa, wakiwa wamezoea mazingira kiukweli wanastahili pongezi.
“Kitu kikubwa wanachohitaji ni fitinesi pekee ambalo lipo chini yake, atahakikisha anawapa mazoezi ya kutosha ili waendane na kasi ya wachezaji wenzao,” alisema Robertinho.