Klabu ya Ruvu Shooting FC ya mkoani Pwani imezitakia kila la heri timu za Simba SC na Yanga SC ambazo zote zinashiriki kwenye mashindano ya Klabu bingwa ambayo inaanza kutimua vumbi leo.

Taarifa ya klabu hiyo iliyotumwa kwenye ukurasa rasmi wa klabu hiyo ulisomeka hivi:

“Ruvu Shooting tunawatakia ushindi wawakilishi wetu katika mashindano ya Kimataifa ya CAFCL, Simba SC na Young Africans SC, katika michezo yao ya leo kwenye hatua ya awali ya CAFCL”

Ruvu Shooting:"Kila la Kheri Simba na Yanga"

Yanga SC watakuwa ugenini kucheza dhidi ya ZALAN FC kutoka Sudan Kusini, lakini mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa taifa wa Benjamin Mkapa majira ya Saa 10:00 Jioni, hii ni kwa sababu za kiusalama hivyo Zalan walichagua kucheza mchezo wao hapa Tanzania.

Ruvu Shooting:"Kila la Kheri Simba na Yanga"

Klabu ya Simba SC nao wameanzia ugenini dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi, mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu nchini Malawi majira ya saa 10:00 Jioni.

Kwa upande wa Simba SC wamepokea salamu hizo kwa kuandika komenti kwamba ‘Asanteni sana Ruvu Shooting’.

Ruvu Shooting:"Kila la Kheri Simba na Yanga"

Nao mashabiki mbalimbali waliopitia ujumbe huo walianda majibu yao kwa mitazamo tofauti.

Ruvu Shooting:"Kila la Kheri Simba na Yanga"

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa