WAKITARAJIA kucheza mechi ya kirafiki leo dhidi ya Kipanga FC, nyota wa Simba, Pape Sakho atakuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mguu.

Mchezo huo wa kirafiki unakuwa wa pili tangu Simba waende Zanzibar kwa kipindi hiki ambacho ligi imepisha ratiba ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

 

Sakho Ana Majeraha Simba

Kwenye mchezo wa kwanza Simba walikipiga dhidi ya Malindi na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Nassoro Kapama.

Akizungumzia hali ya kikosi chao, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa “Wachezaji wana hali nzuri kuelekea mchezo wa usiku dhidi ya Kipanga.

 

Sakho Ana Majeraha Simba

“Anayesumbuliwa na majeraha ni Pape Sakho ambaye aliumia kwenye mchezo uliopita kwahiyo atakosa mechi ya leo na atarejea uwanjani atakapokuwa fiti.”

 

Sakho Ana Majeraha Simba

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa