MCHAMBUZI wa soka nchini Saleh Ally ‘Jembe’ amesema kuwa winga wa klabu ya Yanga Bernard Morrison anatakiwa kurekebisha tabia yake ya kushindwa kujizuia hasira zake na mwishowe kufanya matukio ambayo yamesababisha afungiwe kucheza michezo mitatu ya Ligi Kuu ya NBC pamoja na faini ya shilingi milioni 1.
Akifanya mahojiano na mwandishi wa Global TV amenukuliwa akisema kuwa licha ya kuwepo na taarifa za kuwa na utovu wa nidhamu lakini Morrison ni moja kati ya wachezaji wacheshi sana na wenye roho nzuri hasa pale anapokuwa na wachezaji wenzake tangu akiwa Simba SC na hadi sasa akiwa na klabu ya Yanga.

 

Saleh Jembe: Morrison ni Mtu Poa Sana Ila Abadilike
Bernard Morrison
“Hata ukisema nimpe ushauri ningekuwa nimepata nafasi basi ningesema anapaswa arekebishe hii hali kwa sababu ukiangalia siku ile kwanini amepata hiyo adhabu ni kwa sababu alimkanyaga beki wa Azam ambaye kwake haikuwa na faida yoyote mpira ulikuwa tayari umeshatoka.” amesema Jembe.

Morrison alipata adhgabu hiyo ya kufungiwa kucheza michezo mitatu ya Ligi Kuu ya NBC kutokana na kufanya kosa la kumkanyaga mlinzi wa kulia wa klabu ya Azam Lusajo Mwaikenda katika pambano la Ligi Kuu lililomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 2-2.

 

Saleh Jembe: Morrison ni Mtu Poa Sana Ila Abadilike

Kwa adhabu hiyo Morrison anatarajiwa kuikosa michezo mitatu ambayo ni dhidi ya Ruvu Shooting, Namungo pamoja na mchezo dhidi ya watani wa jadi Simba SC

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa