Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania nahodha Mbwana Ally Samatta ameeleza uchu wake wa kurudi kucheza timu moja wapo ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara.
Ikumbukwe, kuwa Samatta amekuwa kwenye nyakati za mwisho za kucheza soka barani Ulaya na mara zote amekuwa akisisistiza juu ya tamaa yake ya kutaka kustaafia Soka kwenye ardhi ya Tanzania.Samatta anatamani kuja kumalizia soka lake nchini ili kujua namna soka la nchi hii linavyoendelea na mabadiliko yaliyopo kwani kuna mabadiliko makubwa tangu alipoondoka.
Na watu wake wa karibu wamedokeza kuwa, anatamani kucheza soka lake kwenye nyakati za mwisho kwenye moja ya timu za Kariakoo.