Mkurugenzi mwendeshaji wa klabu ya Yanga Senzo Mbatha Mazingiza leo ndio siku yake ya mwisho kuhusu kwa nafasi hiyo kwenye klabu ya Yanga na ameomba kutoongezewa muda wa kuendelea kkufanya kazi na klabu hiyo.
Senzo ni raia kutoka Afrika Kusini, na kwa mara ya kwanza kufanya kazi kwake nchini Tanzania ni alipojiunga na klabu ya Simba Sc kama mkurugenzi mwendeshaji wa klabu hiyo, mwaka 2019 na kuhudumu kwa kipindi kimoja tu, huku akifanikiwa kuipatia klabu hiyo ubingwa wa ligi kuu na kuifikisha robo fainali michuano ya Caf.
Senzo alijiunga na klabu ya Yanga mwaka 2020, kwa mkataba wa miaka miwili ambao unafika tamati hii leo, kwenye miaka miwili aliyodumu kwenye klabu ya wananchi, ameisaidia kumaliza ligi pasipo kupoteza hata mchezo mmoja na kufanikiwa kushinda makombe yote ya ndani ikiwemo NBC Premier League, Azam Confederation na ngao ya jamii.
“Imekuwa miaka mitatu ya kujifunza na kulielewa kwamba soka Tanzania ni dini na linautamaduni wake wa kipeee. Ningependa kuchukua nafsi hii kumshukuru kila mmoja ambae amekuwa sehemu ya kuwa na makazi bora hapa tanzania.
“Asante Tanzania kwa ukarimu. Moja ya nchi bora kwa kupenda soka mara ya kwanza nilijifunza! “Nguvu Moja” na baadae nilielewa “Daima mbele nyuma mwiko” ambapo ndipo palikuwa nyumbani hadi tutakapo kutana tena.
“Miaka yake mitatu aliyokuwepo Tanzania amefanikiwa kuiongoza vilabu viwili ambavyo ni simba na yanga huku akifanikiwa kushinda jumla ya mataji sita kwa ujumla.” Senzo Mbatha Mazingiza
YANGA SC SIMBA SC
2020-22 2019-20
- NBC Premier League Vodacom Premier League
- Azam FA Cup Azam FA Cup
- Community Shield
- Mapinduzi Cup