TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wasichana wa (U17), Serengeti Girls inatarajia kuondoka kesho kutwa Jumapili nchini kuelekea nchini England kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na mashindano ya kombe la dunia yatakayofanyika mwezi ujao India.

 

Serengeti Girls Kutimkia England

Safari hiyo inakuja baada ya timu hiyo juzi Jumatano kufanyiwa hafla ya kuagwa na kukabidhiwa bendera na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa kwenye hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere uliopo Posta Dar.

Serengeti Girls itakaa kambi kwenye mji wa Southampton na wanatarajia kupata nafasi ya kucheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali za wanawake za eneo hilo na miji mingine ikiwa ni sehemu ya kuwaweka sawa wachezaji.

Serengeti Girls Kutimkia England
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake Serengeti Girls Wakishangilia moja ya bao walilofunga ugenini.
Baada ya hapo huenda timu ikasafiri na kwenda Dubai kuweka kambi fupi tena na baada yah apo watavuka moja kwa moja kwenda India kwa ajili ya Kombe la Dunia itakayoanza Oktoba 11 hadi 30.

Tanzania imepangwa kundi D na timu za Japan, France na Canada. Huku karata yao ya kwanza wakiitupa Oktoba 12 dhidi ya Japan, kisha Oktoba 15 dhidi ya France na kumalizana na Canada Oktoba 18.

 

Serengeti Girls Kutimkia England

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa