Shabiki wa Mtibwa Sugar Alambishwa Dozi 3

Shabiki wa timu ya Mtibwa Sugar, Godfrey Damson amefungiwa kuingia uwanjani kwa kipindi cha miezi mitatu (3) kwa kosa la kuwafuata waamuzi waliochezesha mchezo kati ya  Mtibwa Sugar vs Yanga kwenye chumba chao wakati wa mapumziko.

 

Shabiki wa Mtibwa Sugar Alambishwa Dozi 3

Shabiki huyo hakuishia kuwafuata tu, bali aliwatolea matusi na kuwatishia kuwapiga waamuzi hao kwa kudai kuwa hawatendi haki kwa timu yake ya Mtibwa Sugar ambao ulimalizika kwa Walima Miwa hao kupoteza kwa bao 1-0.

Tukio hilo lilitokea kwenye mchezo huo uliopigwa tarehe 31 Desemba 2022 katika uwanja wa Manungu huko mkoani Morogoro huku ikiwa ni mchezo wa pili mfululizo kwa Mtibwa kupoteza.

Shabiki wa Mtibwa Sugar Alambishwa Dozi 3

TFF inasema akuwa adhabu hiyo ni kwa uzingativu wa kanuni ya 47:2 ya Ligi kuu kuhusu udhibiti kwa klabu.

Mtibwa mpaka sasa wanashikilia nafasi ya 8 kwenye michezo 19 aliyocheza na kujikusanyia pointi zake 24.

Acha ujumbe