Mechi iliyokua inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mpira wa miguu Tanzania,Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kati ya Simba dhidi ya Yanga na mchezo huo ukishuhudiwa kumalizika kwa bao moja kwa moja mechi hiyo iliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar-es-salaam.
simba
Mchezo huo ambao ulianza na kasi sana haswa upande wa Simba ambao walionekana kulitafuta bao na mapema kabisa dakika ya 15 Augustine Okrah akiiandikia bao la kuongoza klabu ya Simba.

Mpira uliendelea kua wa kutafutana mpaka pale mchezaji wa Simba Mzamiru Yassin kufanya madhambi ambayo yalisababisha mchezaji wa Yanga Stephane Aziz Ki kupiga mpira wa madhambi kwa shuti kali na kuisawazishia klabu ya Yanga na mchezo huo kwenda mapumziko bao moja kwa moja.simbaKipindi cha pili kilianza kwa timu zote kuonekana kuchez kwa nidhamu na mashambulizi ya kushtukiza kwa pande zote mbili na nafasi kadhaa zikitengenzwa lakini hazikuweza kuzaa mabao katika mchezo huo na kumalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Huku mwamuzi wa mchezo huo Ramadhan Kayoko akizua gumzo kwa namna alivyochezesha mchezo huo, haswa pale ambapo alipokua anatoa kadi za njano katika mchezo huo huku akitoa kadi 5 kwa upande wa Simba huku 4 kwa upande wa Yanga zikiwa zimetoka kadi 9 kwa ujumla katika mchezo huo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa