Hatimaye baada ya kusubiri kwa muda mrefu na kuahirishwa kwa Droo ya mkundi ya CAF, Simba na Yanga hii leo kila mmoja amejua anacheza na nani katika hatua ya makundi atakayocheza.
Simba yeye yupo katika Kundi C ambapo atamenyana dhidi ya Raja Casablanca kutoka Morocco, Vipers ya Uganda na Horoya ya nchini Guinea ambapo kila timu itacheza michezo sita nyumbani na ugenini.
Wakati kwa upande wa Yanga yeye yupo Kombe la Shirikisho na atavaana na TP Mazembe ya Congo, US Monastrienne ya Tunisia, na Real Bamako ya Mali, huku mechi hizo zikitarajiwa kupigwa kuanzia tarehe 12 February 2023.
Simba na Yanga zote zinataka kufanya vizuri kwenye msimu huu huku malengo ya mnyama yakiwa ni kufika hatua ya nusu fainali ambayo hajawahi kufika toka aanze kushiriki mchuano hii mara nyingi huishia robo fainali.
Yanga naye baada ya kuondolewa Klabu Bingwa anataka kufanya vizuri ili aweze kufika mbali kwenye Kombe hili.