Coastal, Simba boli litatembea Mkwakwani

PANDE zote mbili kati ya Coastal Union ambao ni wenyeji na Simba SC ambao ni wageni kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Jumamosi hii kwenye uwanja wa Mkwakwani wamekiri kuwa mpira utapigwa mwingi sana.

Coastal, Simba boli litatembea Mkwakwani

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kocha wa timu hiyo Juma Ramadhan Mgunda anataka kucheza mpira mkubwa kwa kuwa anajua haitakuwa rahisi kwao kupata ushindi mbele ya Coastal Union.

Jonathan Tito ambaye ni msemaji wa timu hiyo naye aliliambia Championi Jumamosi kuwa, timu hizo zinacheza soka linalofanana kwahiyo kutakuwa na burudani ya kutosha kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Ahmed alisema: “Hautakuwa mchezo rahisi kwetu kwa kuwa mara zote tunapokutana na Coastal Union huwa siyo rahisi. Tunaijua timu hii kuwa ina wachezaji bora na wanajua kupambana. Lakini mpango wetu ni kusaka alama tatu.

“Kocha wetu Juma Mgunda anarejea nyumbani na anajua kuwa haitakuwa rahisi kwa kuwa anawafahamu vijana hawa. Hakika boli litatembea Mkwakwani, ila alama tatu ni zetu.”

Coastal, Simba boli litatembea Mkwakwani

Kwa upande wa Tito yeye alisema: “Kupoteza mbele ya Dodoma Jiji kwenye uwanja wetu halikuwa jambo nzuri. Tunahitaji kuutumia mchezo huu wa Simba kurekebisha makosa yetu. Siyo rahisi lakini tunajua vijana wanajua umuhimu wa kushinda mchezo huu.”

Coastal watacheza na Simba jioni ya kesho kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga saa 10 jioni. Mara ya mwisho kucheza na Coastal kwenye uwanja huo msimu uliopita na walishinda mabao 2 – 1

 

Acha ujumbe