Klabu ya Simba leo itashuka dimbani kumenyana na klabu ya Mtibwa Sugar kutoka mkoani Morogoro katika mchezo utakaopigwa ndani ya dimba la Benjamin Mkapa.

Baada ya kufungwa na Azam Fc siku ya alhamisi na kudondosha alama tatu muhimu, Leo hasira zote watazihamishia kwa wakata miwa klabu ya Mtibwa Sugar ambao nao wamekua katika kiwango kizuri siku za hivi karibuni.simbaKlabu ya Simba wataingia uwanjani kuzisaka alama tatu muhimu baada ya kudondosha alama mchezo uliomalizika, Lakini pia kujaribu kupunguza pengo la alama baada ya watani zao kuwaacha kwa alama sita kwasasa baada ya kushinda dhidi ya Geita Gold jana.

Mnyama leo atanufaika katika mchezo huo ambao nyota wake kadhaa wamerejea kama Sadio Kanoute aliokua mgonjwa, Shomari Kapombe ambae pia alikua na majeraha lakini Mzamiru Yassin kurejea baada ya kutoka kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.simbaNahodha wa Simba Mohamed Hussein pia amezungumza na kusema mchezo wa leo ni muhimu na wameyafanyia kazi makosa ambayo yalijitokeza katika mchezo uliopita na kuahidi ushindi katika mchezo wa leo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa