SIMBA ILIVYOGAWA DOZI KIAINA BONGO

Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kimemalizana na wapinzani wao Kilimanjaro Wonders kwa maajabu ya mtoto wa maajabu Chasambi kupachika bao huku David Kameta akitoa pasi mbili za mabao kwenye ushindi wa mabao 6-0 katika mchezo wa CRDB Federation Cup uliochezwa jana KMC Complex Dar.

 

SIMBA ILIVYOGAWA DOZI KIAINA BONGO

Simba walianza kupata bao la mapema kwenye mchezo huo ikiwa ni dakika ya kwanza kupitia kwa mshambuliaji Valentino Mashaka akiwa ndani ya 18 katika sekundi ya 25 kwa mguu wake wa kulia.

Hiyo ilikuwa ni mwanzo kabisa wa mchezo na iliwachukua dakika tatu Simba kufunga bao la pili kupitia kwa kiungo wa maajabu Ladack Chasambi ilikuwa dakika ya nne muda mfupi baada ya Mashaka kuwaondoa mashaka mashabiki wa Simba.

Kabla hawajapoa Kilimanjaro Wonders walikutana na maajabu mengine dakika ya 9 katika harakati za kuokoa hatari ndani ya 18, nyota Patrick Sebastian alijifunga bao likiwa ni bao la tatu.

Joshua Mutale kiungo mshambuliaji wa Simba ambaye alianza kikosi cha kwanza chini ya Kocha Fadlu Davids yeye alifunga bao la nne ilikuwa dakika ya 20 kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup na dakika zilizoongezwa kipindi cha pili zilikuwa ni tatu.

SIMBA ILIVYOGAWA DOZI KIAINA BONGO

Dakika ya 45 ilibaki kidogo Kilimanjaro Wonders kuonyesha maajabu yao kwa kumtungua Ally Salim baada ya nyota wa Okejapha kufanya makosa kwenye kuokoa hatari bahati ikawa kwa Salim kwa kuwa mpigaji alkosa utulivu mpira ukatoka nje ya lango.

David Kameta ambaye alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Kilimanjaro Woders alikuwa kwenye kutimiza majukumu yake alitoa pasi yake ya kwanza dakika ya nne ikakutana na Chasambi.

Kipindi cha pili Kameta alitoa pasi dakika ya 48 ikakutana na Steven Mukwala akaruka juu waaa na bao la sita likifungwa na Edwin Balua dakika ya 79 akitumia pasi ya Mutale.

Acha ujumbe