Kikosi cha Simba kimewasili salama jijini Dar es salaam kikitokea Dodoma ambapo walikuwa na mchezo na timu ya Dodoma Jiji na kufanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa Jamhuri.

 

Simba Imerejea Salama Jijini Dar es salaam

Bao hilo la Simba lilitupiwa kimyani na mshambuliaji mpya waliymsajili dirisha dogo hili la usajili Jean Baleke na kuifanya klabu hiyo ivune pointi 3 muhimu hapo jana huku Dodoma wakiwa wanazidi kuteremka chini kwenye msimamo.

Klabu hiyo baada ya kurejea itakuwa ikijiandaa na mchezo unaofuata ambao watamenyana dhidi ya Singida Big Stars February 3 kabla ya michuano ya CAF ambayo inaanza February 10 ambapo wataanzia ugenini dhidi ya Horoya.

Simba Imerejea Salama Jijini Dar es salaam

Baada ya hapo watarudi Dar kwaajili ya mchezo wa mwingine wa kwenye kundi hilo ambapo watacheza dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco na utapigwa February 17 katika dimba la Benjamin Mkapa.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa