SIMBA INASUKWA UPYA KIBABE ZAIDI

Mwamba Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba ana kibarua cha kusuka upya kikosi hicho kuelekea msimu wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani kitaifa na kimataifa.

SIMBA INASUKWA UPYA KIBABE ZAIDI

Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika itasubiri mshindi wa mchezo kati ya Uhamiaji dhidi ya Libya kwa kuwa haitaanzia hatua ya awali.

Mbali na Msimbazi kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, Coastal Union pia ipo anga la kimataifa baada ya kugotea nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Mnyama amesema: “Kocha Fadlu anatambua kitu ambacho Wanamsimbazi wanahitaji hivyo anasuka kikosi kazi kwa ajili ya kuleta ushindani akishirikiana na benchi zima la ufundi.”

SIMBA INASUKWA UPYA KIBABE ZAIDI

Wachezaji wapo tayari wanaendelea na mazoezi na wapo wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi kwa msimu wa 2023/24 tunaamini kwamba tutafanya vizuri mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.

Acha ujumbe