Ahemed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba ameweka wazi kuwa usajili wao mpya wa Ellie Mpanzu umejibu kwa haraka licha ya kuwa na mchezo mmoja wa ushindani.

Nyota huyo mchezo wake wa kwanza ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar ambapo kwenye mchezo huo alikomba daika 57 alikuwa na uwezo wa kupiga mashuti ya mbali na spidi ndani ya uwanja.
Katika mchezo huo uliochezwa Desemba 21 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 2-5 Simba ukiwa ni ushindi mkubwa kupatikana ndani ya msimu wa 2024/25.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Ally amesema hakuna ambaye anaubeza uwezo wa Mpanzu kutokana na mwanzo alioanza nao atafanya makubwa ndani ya Simba.



