SIMBA KAZI SIO NYEPESI DHIDI YA AHLY MISRI

KLABU ya Simba kutoka Tanzania inajiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly unaochezwa wiki hii huko Misri.

Mchezo ambao kimsingi hautakuwa rahisi kwa Sababu Wanakwenda Cairo Misri wakiwa wametanguliwa bao 1-0, Baada ya kukubali kichapo hicho wakiwa Tanzania wiki iliyopita.SIMBAMbele ya Al Ahly, Simba walipoteza nafasi nyingi na mwisho kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Mkapa huku Kibu Dennis akiwa katika ubora akiwa na kila kitu kasoro umaliziaji tu hapo ndo pasua kichwa.

Simba wanakazi ngumu yakufanya kimataifa kwa kuwa wanatambua Al Ahly wakiwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huwa wanabadilika ni kweli huwa wanabadilika kuanzia mbinu mpaka mipango.
Baada ya kufungwa dakika ya 5 Simba walikosa mbinu ya kuwafungua Al Ahly ambao ni mabingwa watetezi.

Namna Simba walivyoamua kuwakabili wapinzani wao walikuwa na presha kubwa huku pasi nyingi walizokuwa wakipiga zikiwa hazina faida na hata mikimbio kwenye nafasi bado ilikuwa shida.SIMBAWalikuwa na nafasi ya kuimaliza mechi kwa Mkapa katika nafasi saba zililenga lango lakini mlinda mlango wa Al Ahly alikuwa kikwazo.
Aprili 5 2024 mchezo unatarajiwa kuchezwa robo fainali ya pili Misri huko balaa linatarajiwa kuwa zito.

Acha ujumbe