Mabosi Simba SC Yampa Dau Nono Kuingo wa Geita Gold

Zikiwa zimebaki siku chache kuelekea kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili mwezi Januari, tayari taarifa za baadhi ya wachezaji kutoka timu mbalimbali wameanza kuhusishwa kuhitajika na timu nyingine ikiwemo klabu ya Simba SC, ambayo imekuwa ikihusishwa sana na usajili wa dirisha dogo ili kuziba mapengo kwenye baadhi ya nafasi.

 

simba

Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo na Uongozi wa Geita Gold FC ili kupata saini ya kiungo mkabaji Kelvin Nashon kinda mwenye umri wa miaka 22.

Kelvin Nashon ni kinda anayeonekana kufanya vizuri kwa sasa ndani ya kikosi cha Geita Gold FC

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo Zainab Rajab anasema “tayari Ma bosi wa Simba SC wametenga donge kwa ajili usajili wake kipindi cha dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Januari15”

 

simba

Simba watamsajili Kelvin Nashon kama mbadala wa Mzamiru Yassin pamoja na Sadio Kanoute kutokana na umri wake kuwa bado mdogo na kiwango chake kuonekana bora.

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

Acha ujumbe