Klabu ya Simba kesho watashuka dimbani kukabiliana na klabu ya African Sports kutoka mkoani Tanga katika mchezo wa kombe la Azam Federation hapo kesho.
Simba watashuka dimbani kumenyana na African Sports wakiwa na kumbukumbu nzuri baada ya kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Vipers ya nchini Uganda ambapo ulipigwa nchini Uganda jijini Kampala, Ikiwa ni baada ya ya kucheza michezo mitatu mfululizo bila matokeo ya ushindi.Kocha wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Brazil Robertinho ameahidi ushindi kuelekea mchezo huo dhidi ya African Sports katika kombe la shirikisho la Azam, Kwani itakua ni vizuri kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Vipers kwajili ya kuendeleza morali ya ushindi.
Kocha Robertinho vilevile alieleza katika mchezo wa kesho dhidi ya klabu ya African Sports wamepanga kupata alama tatu muhimu, Lakini watahakikisha wanawapa nafasi wachezaji ambao wamekua hawapati nafasi mara kwa mara kikosini hapo kwani kuna mchezo mgumu unawakabili siku chache zijazo nao ni dhidi ya klabu ya Vipers mchezo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.Klabu ya Simba wanautolea macho zaidi mchezo wa marudiano dhidi ya klabu ya Vipers na hiyo ndio sababu ya kocha Robertinho kusema wanatarajia kuwapa nafasi zaidi wachezaji ambao wamekua hawapati nafasi klabuni hapo mara kwa, Mnyama anahitaji alama sita ili aweze kukaa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.