Klabu ya soka ya Simba leo itajitupa uwanjani katika dimba la Benjamin Mkapa kukabiliana na klabu ya Ihefu kutoka jijini Mbeya katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara.

Klabu ya Simba leo watajiuliza leo dhidi ya Ihefu baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars siku ya jumatano katika dimba la Liti mkoani Singida.simbaMchezo wa leo kwa wekundu wa Msimbazi ni wa muhimu zaidi kushinda kwani mpaka sasa wako nyuma ya klabu ya Azam Fc na mabingwa watetezi watani wao klabu ya Yanga ambao wanaongoza ligi wakiwa na michezo miwili mkononi.

Mnyama pia leo atakua na faida baada ya mchezaji wake nyota raia wa Ghana Augustine Okrah kurejea kwenye mchezo wa leo ambapo alikosekana katika mchezo uliopita dhidi ya Singida Big Stars.simbaKlabu ya Simba leo itaendelea kukosa huduma ya Mchezaji wake nyota Claotus Chama ambaye anatumikia adhabu na huu utakua mchezo wake wa pili baada ya kufungiwa na bodi ya ligi kutokana na kosa la kutopeana mikono na wachezaji wenzake kwenye mchezo wao na Yanga.

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa