Kuelekea siku ya Simba Day, hii leo klabu hiyo ambayo makazi yake yapo Msimbazi wametangaza kuwa siku ya tarehe 6 Agosti watakapokuwa wakiadhimisha siku yao watamenyana dhidi ya Power Dynamos.
Taarifa hiyo imetolewa leo hii na Afisa habari wao Ahmed Ally huku wakisema kuwa siku hiyo itakuwa ni ” Unyama Mwingi”, siku ya mnyama, huku kukiwa na shangwe na furaha kwa mashabiki wa mnyama.
Ikumbukwe kuwa Dynamos ndio mabingwa wa Ligi kuu ya Zambia msimu uliopita huku wakitarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na vijana wa Robertinho siku hiyo.
Simba wanatarajia kujiandaa na msimu mpya baada ya kukosa taji la ligi kuu mara mbili mfululizo mbele ya wapinzani wao Yanga wao. Hivyo msimu huu wanasema wamejiandaa kufanya maajabu.
Mpaka sasa klabu hiyo imefanya usajili wa wachezaji mbalimbali akiwemo Aubin, Che Malone, Onana, Jefferson Luis, Fabrice Ngoma, Hamis Abdalla, Chilunda pamoja na kumrudisha aliyekuwa mchezaji wao Luis Jose Miquissone.