Ligi kuu ya NBC Tanzania inatarajiwa kuendelea hii leo kwa michezo miwili ambapo mchezo wa usiku utakuwa ni kati ya Simba SC dhidi ya Mashujaa kutoka kule Kigoma ambao wapo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi.
Mchezo huo utapigwa majira ya saa 2:15 usiku katika dimba la Chamazi Complex ambapo Mnyama baada ya kutoka kushinda mchezo wake uliopita atakuwa akihitaji pointi zingine za kujiweka vyema kwenye msimamo wa ligi.
Simba yupo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi zake 18 akishinda mechi zake 13, sare tatu na kupoteza michezo miwili hadi sasa na kufanikiwa kujikusanyia pointi zake 42.
Huku Mashujaa yeye akiwa amekusanya pointi zake 21, akishinda mechi zake tano, sare sita na kupoteza mara tisa hadi sasa.
Mara ya mwisho timu hizi kukutana, vijana wa Benchika walishinda kwa mbinde sana. Je leo hii Wekundu wa Msimbazi wanaweza kuondoka na pointi tatu kirahisi mbele ya Mashuijaa?. Mechi hii imepewa ODDS 1.19 kwa 10.78 Meridianbet.