Simba Kumenyana na Raja Casablanca Saa 7 Usiku Leo

Michuano ya klabu bingwa kuendelea hii leo kwenye viwanja mbalimbali, ambapo klabu ya Simba itakuwa ugenini kukichapa dhidi ya Raja Casablanca kwenye mchezo wao wa marudiano.

 

Simba Kumenyana na Raja Casablanca Saa 7 Usiku Leo

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 7:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki wakati kwa upande wa Morocco mchezo huo utakuwa ni saa 5:00 usiku huku kila timu ikijiandaa kupata ushindi huo.

Timu zote mbili Simba pamoja na Raja Casablanca zimeshafuzu hatua ya robo fainali huku Casablanca akiwa hajapoteza mchezo wowote toka mashindano haya yaanze na ndiye kinara wa kundi hilo.

Mechi ya kwanza walipokutana, Robertinho alipoteza kwa mabao 3-0 akiwa nyumbani katika dimba la Benjamin Mkapa. Je hii leo ataweza kulipiza kisasi kwa Raja ambaye anaonekana kuwa bora na imara?

Simba Kumenyana na Raja Casablanca Saa 7 Usiku Leo

Kiungo wa Wekundu wa Msimbazi Saido Ntibanzokiza amesema kuwa wamejiandaa kupata ushindi licha ya uchovu wa safari lakini pia wanahitaji kufika mbali kwenye michuano hii.

Beki wa Msimbazi Mohamed Hussein anasemekana kuwa ataukosa mchezo huo baada ya kupata kadi za njano tatu mfululizo hivyo leo hii kocha Robertinho ataamua ataanza na nani.

 

 

Acha ujumbe