SIMBA KUTUMIA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID ARUSHA

TAARIFA za ndani kabisa kutoka klabu ya Simba ni kwamba vongozi wa Simba wanafikiria kuhamishia mechi zao za nyumbani msimu ujao 2024/25 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

 

Habari zinasema asilimia kubwa ya uongozi wanalijadili hilo, na kwamba Dar es Salaam wamepanga kuchezea mechi zao za Kombe la Shirikisho tu.

 

Za ndani kabisa zinasema kwamba wanaona kama Dar es Salaam pamekuwa pagumu kwao katika misimu ya hivi karibuni kwani kumekuwa na mambo mengi.simbaSimba wanaamini kwamba pia Arusha kuna mashabiki wao wengi na hata miundombinu ya viwanja vya mazoezi na kambi ni rafiki.

 

Ingawa lolote linaweza kutokea watakaporudi kwenye kambi ya mazoezi nje ya nchi, lakini mpaka sasa wameanza kuwasiliana na mamlaka za Arusha kuona jinsi ya kuuboresha uwanja wa Arusha.

 

Mchezo wao dhidi ya KMC FC waliupeleka Arusha na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Bao lililofungwa Saidoo Ntibazonkiza mapema kabisa kipindi cha kwanza.

 

Kwa upande wa hapa Dar Es Salaam kuna viwanja vichache na timu ziko nyingi, uwanja wa Azam FC unatumika na Azam FC, na watani zao Yanga wanautumia na wanapata matokeo mazuri tu.

 

Mashabiki wa Mnyama wamekuwa wakisema kwamba uwanja wa Azam FC ni mgumu sana kwao, kwani kuna mambo umefanyiwa na watani zao hivyo wanapocheza wao kupata matokeo ni ngumu tofauti na uwanja wa Uhuru au Benjamin Mkapa.

 

Awali Simba walikwa wanatumia uwanja wa Uhuru kabla ya uwanja huo kufungiwa na TFF kwa kuwa umechoka na unahitaji maboresho makubwa, upande wa pichi na sehemu za kurushia matangazo.simbaUwanja wa Benjamin Mkapa bado unaendelea na ukarabati mkubwa na utatumika tu kwa mehi kubwa, tofauti na hapo hautatumika mpaka maboresho yatakapokamilika.

 

Uwanja wa Kinondoni Mwenge umekamilika na upo tayari kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu msimu ujao, utatumiwa na KMC FC, lakini kikwazo pekee cha uwanja huo kwa Simba ni majukwaa ya mashabiki, unabeba mashabiki wachache sana, hali itakayopelekea Simba kupoteza mapato ya viingilio.

Acha ujumbe