TAMASHA kubwa la mpira wa Miguu Tanzania na Afrika kwa sasa ‘Simba Day‘ mwaka huu litafanyika Agosti 3 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam badala ya Agosti 8 kama ambavyo imezoeleka kila msimu.
Tamasha hilo ambalo limekuwa maarufu nchini limepangwa kufanyika Agosti 3 kutokana na ratiba ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inayohusiana na mechi za Ngao ya Jamii itakayopigwa kati ya Agosti 8-11.Akizungumza jijini Dar es Salaam Ijumaa (Juni 28), Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kutokana na kuwepo kwa michuano ya Ngao ya Jamii siku hiyo wameamua kurudisha siku nyuma.
“Kabla ya kilele chake kutatanguliwa na Wiki ya Simba itakayoanza Julai 24 ambayo itakuwa na matukio mbalimbali ya kijamii kama kuchangia damu na (watu) wenye mahitaji maalumu,” amesema.