Nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Azam inatarajiwa kupigwa hii leo ambapo itakuwa ni kati ya Simba dhidi ya Azam FC ambao utapigwa majira ya saa 9:30 mchana.

Nusu fainali hiyo itapigwa katika dimba la Nangwanda Sijaon Mtwara, huku mwamuzi wa mchezo huo atakuwa ni Tatu Malogo kutoka Tanga ndiye atakayeongoza jahazi hilo hadi kipyenga cha mwisho cha mchezo.
Kila mashabiki na wasemaji wa timu wanatamba kwelikweli kuelekea nusu fainali hiyo kila timu ikijiamini kuondoka na ushindi na hatimaye kuingia fainali ya Kombe hili ambalo huhusisha timu hadi daraja la kwanza.
Mara ya mwisho kukutana kwenye Simba na Azam kwenye FA Wanalamba lamba walifungwa bao moja mbele ya mnyama. Na leo wanataka kulipiza kisasi lakini je wataweza kulipa hicho kisasi?.

Timu hizi kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC wanapisha pointi 11 huku mechi mbili za mwisho walizokutana kwenye ligi Matajiri wa Chamazi wameondoka na pointi 4 huku mechi ya kwanza mnyama alipoteza na ya pili walitoa sare.

